ROBOTI WA KIKE ANATISHIA UWEPO WA MAHUSIANO YA KIMAPENZI
Teknolojia inazidi kwenda Kasi Sana binadamu anazidi kugundua vitu vya kustaajabisha vingine unaweza ukasema ni vizuri na kwa upande mwingine unaweza ukasema ni vibaya.
Jambo ambalo linawashtua wengi Sana ni kugunduliwa kwa roboti wa kike(mwanamke) ambapo atakuwa na sifa Kama za mwanamke zote baadhi ya sifa hizo ni kufanya mapenzi na mwanaume, kuwa na siku zake, kufanya kazi za nyumbani,
Roboti huyo anayetumia nishati ya umeme yaani chaji inayotokana na umeme wa kawaida pamoja na nishati ya jua. Watu wamekuwa na maoni mbalimbali kuhusu teknolojia hii.
IDADI ya watu wengi wanasema teknolojia hiyo haifai kwani inakuja kupunguza thamani ya mwanamke endapo teknolojia hiyo itasambazwa utafanya baadhi ya watu wasioe kwa sababu ya roboti huyo amabaye anaonekana kuwa na sifa zinazokaribiana KUFANANA na za mwanamke.
Wapo baadhi ya watu wachache wanaotetea kuwa teknolojia hiyo ni nzuri. Kundi hili linajumuisha Sana vijana ambao hawajaoa ambapo wanaona kuwa roboti huyo anaweza akaondoa changamoto za kupoteza hela kwa kuwa roboti huyo hali, haihitaji mavazi mengi endopo chaji itakuwepo tu ndo gharama yake.
Je wewe upo upande gani hapo je unaunga mkono teknolojia hii Kama ndiyo au hapana tunaomba uache komenti hapo chini kuwaelewesha watu kuhusu teknolojia hii.
Comments
Post a Comment