MWANAMKE ANAEYEDAIWA KUBAKWA NA TRUMPU AANZA KUTOA USHAHIDI
Raisi wa awamu iliyopita wa marekani Donald Trumpu anaendelea kukabiliwa na mashtaka mbalimbali mojawapo ya mashtaka yanayo mkabili ni pamoja na Hili la suala la ubakaji.
Mwanamke E. Jean Carroll siku ya jumatano alifika katika mahakama ya New York akiwa anapeleka mashtaka katika mahakama hiyo ambapo anadai kuwa aliye kuwa raisi wa marekani Donald Trump alimbaka mwanamke huyo miongo mitatu iliyopita katika chumba Cha kubadilishia nguo.
E. Jean Carroll anasema alibakwa na Donald Trump mnamo mwaka 1996. Alipofika katika mahakama alisema maneno haya kwa kumnukuu alisema hivi " nimefika hapa kwa sababu Donald Trump alinibaka. Na nilipoandika mashtaka kwa Mara ya kwanza alikataa na kusema ni uongo. Amedanganya na ameharibu heshima yangu nipo hapa kwaajili ya kuirudisha heshima nilipoteza" alisema mwanamke huyo.
Comments
Post a Comment